Askofu wa jimbo katoliki la Ngong John Oballa Owaa ametataka makleri na majandokasisi kukana ya malimwengu kwa kujisadaka bila kujibakisha kama njia moja ya kudhihirisha imani yao.
Akihubiri katika misa ya nadhiri ya kwanza ya watawa wa missionary sisters of evangelization eneo la Karen jijini Nairobi askofu Oballa amewataka watawa hao siku zote kutilia maanani sala kama ngao ya kukabiliana na jinamizi ya malimwengu ambayo anasema kuwa mara nyingi huyumbisha imani ya watendakazi katika shamba la bwana.
Askofu huyo kadhalika amewataka watawa hao kujitolea na kuweka matumani nyusoni mwa wale watakaotangamana na kuwahudumia kila watakapotekeleza majukumu yao, akisema kuwa wito huo una changamaoto sawia na zile zinazokumba walei.