Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ameandaa mkutano na sekretarieti ya jimbo ili kuweka mikakati maalum ya kutekeleza sinodi.
Katika kikao hicho kilichowaleta pamoja idara mbalimbali ndani ya sekretarieti ya jimbo, askofu Kimengich ametoa wito kwa sekretarieti kuwa mabalozi kamili ya jimbo kwa kusukuma na kuhakikisha kuwa ruwaza ya jimbo inaafikiwa kupitia kwa utekelezwaji ya yale yalioyomo kwenye sinodi.
Mkutano huo ambao ulijumuisha idara mbalimbali jimboni imeandaliwa kwa lengo la kuwahamasisha wale wanaofanya kazi katika idara hizo kujua na kutambua jukumu lao na yale wanaotakiwa kuwajibikia kama inavyonogeshwa kwenye sinodi.
Ikumbukwe kwa askofu Dominic Kimengich tayari amabuni maeneo matatu ya kipastorali na kuwateua mapadre wakuu watakaosimamia kila eneo la kipastorali.