Makala ya nne ya Eldocity Marathon kuandaliwa tena

Mashindano ya mbio za masafa marefu ya Eldoret City Marathon awamu ya nne inatarajiwa kurejelewa tena baada ya mapumziko ya mwaka mmoja huku waandalizi wakieleza kwamba kila kitu kiko shwari.

Akizungumza na wanahabari mjini Eldoret msimamizi wa makala hayo Moses Tanui amesema kwamba chini ya siku kumi zijazo mashindano hayo yataandaliwa mjini Eldoret, huku mashindano hayo yakiwavutia wanariadha wa humu nchini na wa kimataifa.

Tanui vilevile amesema kwamba wataendelea kutumia mifumo za kisasa za kielektroniki huku akibaini kwamba hadi wa sasa idadi inayoridhisha ya wanariadha wamejitokeza na kujisajili.

Msimamizi huyo amewarai wanariadha kuepuka masaa za mwisho kujisajili iwapo wana nia ya kujiunga na wanariadha wengine kwa mashindano hayo akiwaeleza kwamba huenda ndoto zao za kuingia kwenye kumbukumbuku za mbio hizo zikazimwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *