NCCK wataka serikali kutekeleza hitaji la thuluthi mbili.

Muungano wa makanisa nchini NCCK umetoa wito  kwa serikali kuhusisha umma kikamalifu kwenye mdahalo unaoendelea katika ukumbi wa Bomas ili kuafikia kipengee cha kikatiba kilicho na hitaji la umma kuhusishwa.

Katika kikao na wanahabari muungano wa makanisa nchini NCCK umekariri kuwa pendekezo la kuafikia thiluthi mbili ya uwakilishi katika bunge, unastahili maoni ya washikadau na umma wakitoa wito kwa serikali kuweka bayana kwa umma mikakati imeweka ili kuafikia hitaji hili.

NCCK kadhalika umepuuzilia kubuniwa kwa wadhifa ya waziri mwenye mamalaka makuu wakisema kuwa afisi ya musalia Mudavadi si halali kikatiba badala yake wametaka kubuniwa afisi ya kiongozi wa upinzani nchini kama njia moja ya kupata nguvu ya kukosoa serikali kikamilifu.

Haya yanajiri huku jopo lisilo na miegemeo likianza kusikiza maoni ya umma na mashirika mbalimbali kabla ya kuafikia mswala ya kimsingi.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *