Viongozi mbalimbali kwenye kaunti ya Uasin Gishu wametoa hisia zao siku moja tu baada ya bunge la seneti kuidhinisha mji Eldoret kuwa jiji la tano nchini.
Wakiongozwa na mbunge mteule katika chama cha UDA Joseph Wainaina amekaribisha hatua hiyo, akisema kuwa jiji la Eldoret sasa litavutia wawekezaji wengi, akitoa wito kwa serikali ya kaunti ya Uasin gishu kupewa mazingira safi kisheria, badala ya kuweka sheria ambazo zitawafukuza wawekezaji.
Kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta Wainaina amewataka wakenya kuwa na subira, kwa kuwa serikali I mbioni kutatua hali hii, ambayo kwa sasa imepelekea kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu nchini.
Kadhalika ametoa wito kwa serikali kupitia kwa wizara ya kilimo kuweka mikakati na sera maalum, ambayo itapelekea wakulimu kuuza mazao yao bila kuingiliwa na wakiritimba, ambao anasema kuwa huchafua soko la wakulima hasa wa zao la mahindi.