Askofu mkuu wa kiangilikana nchini Jackson Ole Sapit amewataka wanasiasa kutambua kwamba kanisa linajitokeza kila muda kutoa sauti yake kwa maswala kadhaa wa kadhaa kwa lengo la mshikamano wa taifa na wala sio kwa miegemeo yoyote ya kisiasa.
Akizungumza katika parokia ya St.Peter’s Chepng’omi Kimaaam Kaunti ya Nandi,alisema kwamba mara nyingi wanasiasa wanahisi kwamba viongozi wa dini wanaegemea upande wowote akisema wanasiasa wanapokosolewa na viongozi wa dini ni kwa kuwa wamekwenda kinyume na mafundisho ya kidini kupitia matamshi yao akisema taifa hili linaongozwa na mafundisho ya kristu.
Alisisitiza umuhimu wa viongozi kuheshimu uamuzi wa wananchi pindi uchaguzi unapotamatika ndipo taifa liweze kusonga mbele kiuchumi,huku akiwaomba wanasiasa ambao hawajaridhika na uamuzi wa wakenya kufuata njia mbadala za kisheria kutatua malilio yao.
Askofu huyo alitumia fursa hiyo kuwarai wazazi kuwa makini na namna wanavyo walea wana wao kwa kile alisema kuwaingiza kwa matumizi ya simu wakiwa wangali wadogo huenda ikawaathiri kimawazo na hata kimasomo