Dini yakataa LGBTQ Kenya

Viongozi wa dini la Kiislamu kaunti ya Uasin Gishu wametishia kuongoza Maandamano ya kushinikiza mahakama kuu nchini kubatisha uamuzi wake wa kuwaruhusu watu wa mahusiani ya jinsia Moja kutangamana.


Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la maimamu kaskazini mwa Bonde la Ufa Sheikh Abubakar Bini wanasema hatua hiyo haistahili na inaelekeza taifa pabaya Kwa kile wanasema inahujumu amri za mungu.


Wakizingumza Mjini Eldoret viongozi hao wanasema kwamba wataongoza Maandamano ijumaa hii ikiwa hatua ambazo wanasema za kwanza kushinikiza kubatilishwa Kwa uamuzi huo kwani wanadai kwamba mungu wanadamu wanaruhusiwa kuingia kwenye mahusiano iwapo ni WA jinsia tofauti na sio ule WA jinsia Moja.


Wamesema wanahofia huenda taifa hili likajiingiza kwenye misukosuko yasiyokuwa na mwisho iwapo watamkosea mungu kupitia uidhinishaji huo.
Sasa wanamtaka rais William Ruto kujitokeza na kutoa mwelekeo wakieleza kwamba wanaimani taifa hili linaongozwa na Sheria iliyobora ya mola.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *