Unyakuzi wa ardhi ya Soko Shauri Moyo

Wenyeji katika mtaa wa Shauri Moyo viungani mwa mji wa Eldoret wametoa wito kwa serikali ya kitaifa na ya kaunti kuingilia kati na kuwasaidia kupata haki waweze kurejeshewa ardhi hiyo.

Wakaazi hao walisema kwamba ardhi hiyo iliyotengwa kwa minajili ya kujengwa kwa Soko eneo hilo ila wanadai imenyakauliwa na mabwenyenye.

wakizungumza na wanahabari wakaazi hao wamelalamikia baadhi ya mabwenynye kuchukua ardhi hiyo ambayo inatumika na wakaazi kama soko jambo wanalodai kuwa liingiliwe kwa haraka.

Sasa wanatishia kuandamana hadi pale haki itakapotendaka na wahusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria wakisema kwamba walitegemea kwa ukamilisho wa soko hiyo utawawezesha kujikimu kimaisha na kuondoa umaskini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *