Bishop Kimengich; Kumbatieni msamaha

Wakristu wameshauriwa kuwa wenye moyo mwepesi wa kuwasamehe wengine kwa kuwa kila mwanadamu ana upungufu kwa njia tofauti.

Akihubiri wakati wa ufunguzi rasmi wa parokia ya St.Raphael Taito  Nandihills askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amesema kwamba njia pekee ya wanadamu wanaweza kutangamana kwa njia inayostahili katika jamii ni kupitia msamaha.

Amesema kwamba mambo ni mengi katika dunia iliyojaa pilkapilka za maisha na mara si moja huenda watu wakavuka mipaka na kuwakosea wengine hivyo haja ya wao kusameheana.

Askofu Kimengich amesema kwamba ili mwanadamu aweze kuridhi ufalme wa mbingu maswala yanayoweza kuwafungia nje kama vile kukosa kuwasamehe wengine wanapaswa kujitenga navyo na kuwaruhusu wenzao kuwa huru mbele zake mwenyezi mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *