Ulimwengu ukisherehekea siku ya kuhamasisha umma dhidi ya hulka ya kujitia kitanzi,afisa mkuu wa hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi Eldoret Dkt.Wilson Arawasa amesema kwamba visa vingi vya maafa duniani huchangiwa na watu kujiua swala analosema kwamba sharti sera za kudumu kutoka kwa wizara ya afya ziwepo kukabili maswala hayo.
Akizungumza mjini Eldoret Arwasa amesema zaidi ya watu elfu mia Saba kila mwaka wanajitoa uhai duniani akitaka jamii kuwa mstari wa mbele kuwasaidia wale wanaoonekana kuwa na msongo wa mawazo au hata aina yoyote ya ugonjwa wa kiakili akieleza imechangia watu kujitoa uhai.
Afisa huyo vilevile alisema baadhi ya vyanzo vyanzo vya watu kujitoa uhai ni pamoja na kuwa msongo wa mawazo,unyanyapaa na maswala mengine katika jamii akiomba watu kuwa na uwazi kujitokeza wanapokabiliwa na ugumu ndipo waweze kupewa mwelekeo bora.
Kwa upande wake,mwakili kike kaunti ya Uasin Gishu Gladys Boss Sholei alisisitiza haja ya wakenya kupewa hamasisho la kutosha kujitenga na maafa ya kujitoa uhai akisema yanachangiwa na baadhi ya maswala mengi katika jamii.