Naibu rais Rigathi Gachagua ametoa wito kwa magavana nchini kuhakikisha kwamba wakulima wanapata mbolea ya bei nafuu kwa muda unaostahili katika awamu ya pili ya usajili wa wakulima kupokea mbolea ya bei nafuu.
Akizungumza katika kaunti ya Kericho Gachagua alisema kwamba sekta ya kilimo ndio sekta ambayo itawaokoa na kuwasaidia wakenya kujikomoa kwenye lindi la njaa na hivyo haja ya kuimarishwa na kwa wakulima kupata mazao ya kutosha taifa na hata kujikimu wao kibinafsi.
Wakati huo,Gachagua alisema kwamba serikali imeweka mpango wa kutosha kuwawezesha wananchi wenye hitaji kwenye mpango wa inua jamii akisema kwamba kila mkenya ambaye ako kwenye kitengo hicho amepata pesa hizo.
Naibu huyo ametoa onyo kali kwa wale watakaopatikana wakitumia vibaya nafasi zao za kuwasajili wakenya kwa mpango wa inua jamii kwamba watakabiliwa ipasavyo.