Afya bora bondeni

Wizara ya afya katika kaunti ya Elgeyo-Marakwet imeafikiana kushirikiana na hospitali ya misheni ya Kapsowar kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu bila malipo kwa bonde la Kerio.

Akizngumza na wanahabari Dkt.Billy Rodis wa hospitali ya Kapsowar amesema ni njia mojawapo ya kuimarisha huduma za afya zitaimarika na kuwasaidia wenyeji kupata matibabu karibu nao.

Kwa upande wake,afisa mkuu wa afya kaunti hiyo  Jeremiah Chirchir alisema hatua hiyo itaboresha matibabu kwa kuwa shughuli za matibabu zimeathirika kwa muda mrefu kwa sababu ya utovu wa usalama ila kwa sasa huduma hizo zitaimarika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *