Seneta anasakwa na maafisa wa polisi

Seneta wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mnadago na maafisa wengine watatu wakuu kaunti ya Uasin Gishu wameagizwa kufika katika afisi za idara ya upelelezi DCI Nakuru kufuatia sakata inayozingira masomo ya Ughaibuni.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ameamuru kukamatwa kwa Seneta wa Uasin Gishu Jackson Mandago na wengine watatu kuhusu Mpango wa Elimu ya Nje wa Finland na Kanada.

Seneta huyo pamoja na maafisa wengine watatu wakuu wa kaunti, wanasakwa na polisi ili kufunguliwa mashitaka kuhusu sakata ya ufadhili wa masomo katika kaunti hiyo.

Maafisa hao ni Joseph Kipkemoi Maritim, Meshak Rono na Joshua Kipkemoi Lelei.

Wanahitajika kuandikisha taarifa kuhusiana na ufujaji wa pesa zaidi ya shillinigi billion 1.1 zilizostahili kufadhili wanafunzi wa Finland na Canada.

Wanne hao walistahili kufika kwa DCI kabla ya saa tano asubui huku seneta Mandago akikana kupokea ripoti hiyo kwani amesema kwamba hajapaswa habari hiyo na yuko tayari kufika kwa DCI kuandikisha taarifa yake wakati wowote akiitwa.

Ikumbukwe kuwa seneta Mandago akiwa na wenzake walianzisha mradi wa kuwaeleka ughaibuni wanafunzi na kuwaitisha pesa za masomo hayo kwa ufadhili wa serikali yake kwa wakati alikua gavana na miaka miwili zilizopita wanafunzi wengi wamesalia nyumba ingawa wazazi walidai kulipa mamilioni ya pesa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *