KCCB:masomo ya ngono iondolewa shule za msingi

Baraza la maaskofu wa katoliki nchini KCCB linapendekeza kuondolewa kwa ujumuishaji wa masomo ya ngono shuleni kwenye vitabu vya gredi ya saba mara moja.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa Elimu kwenye baraza hilo ambaye ni askofu wa Jimbo katoliki la Wote Paul Kariuki NJiru wanasema kwamba iwapo wizara ya Elimu itaidhinisha mafunzo hayo ni kama njia moja ya kuhalalisha visa vya wanafunzi kujihusisha kwenye mapenzi ya kuholela na kuchangia hata uavyaji wa mimba.

Maaskofu hao walieleza hofu yao kuu kwamba huenda ujio wa mafunzo hayo yakawaweka kwenye hatari watoto na kuielekeza kizazi kijacho kwenye njia isiyostahili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *