Familia uti wa jamii

Ipo haja ya wanajamii kuhamasishwa vya kutosha kuhusiana na umuhimu wa kukuza familia zao kwa msingi uliodhabiti.

Akiongea katika parokia ya St.Claver Ndalani,askofu wa jimbo katoliki la Machakos Norman King’oo ametaja umuhimu wa jamii kulinda familia zao dhidi ya ,mawimbi ya maisha ndipo familia hizo ziweze kuwa na mwelekeo uliobora katika maisha ya baadae.

Alisema kuwa familia ni chanzo cha miito mbalimbali katika jamii iwe wale wanaotaka kuhudumu katika shamba la bwana kama makleri au majandokasisi au hata taaluma mbalimbali za maisha,yapasa jamii kuwa mstari wa mbele kukuza familia zao na kuwezesha kusimama imara.

Alieleza kwamba viongozi wa maisha za baadae wanatoka katika familia na hivyo watoto wanapaswa kuelekezwa vyema katika maisha yao ya kila wakati kando na kuwajengea imani iliyo dhabiti katika kristu.

Vilevile,askofu huyo aliwataka kina mama kuwa msingi bora kwa wanao na wasije wakawakwaza waume zao akitaja kuwa pindi baba katika familia anapohisi kutengwa familia itaporomoka akieleza haja ya ushirikiano bora kati ya mama na baba na pia watoto kuiwezesha familia hiyo kusimama imara.

Kadhalika,aliwataka watoto kuwa watiivu kwa wakubwa wao hasa wazazi wao maana ni kupitia hilo watajiweka salama kumiminiwa Baraka kutoka kwa mwenyezi mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *