Kampeni ya Amani yazinduliwa

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB umezindua mikakati inayonuia kuleta amani na maridhiano katika majimbo yake sita ambayo yameathirika na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo mkurugenzi wa idara ya sheria za kanisa katika  baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB padre Ferdinand Lugonzo amesema kuwa ushirikiano huu utaleta majimbo yote sita kupitia idara mbalimbali za haki amani na maradhiano kama njia moja ya kuleta uwiano kwenye maeneo athirika

Naye mwenyekiti wa idara ya haki na maridhiano katika baraza hilo ambaye pia ni askofu wa jimbo katoliki la Ngong askofu John Oballa Owaa ameriri haja ya kuwepo kwa usawa katika ugavi wa rasilimali alisema kuwa hii ni mojawapo ya maswala ambayo yamechangia machafuko hao.

Nao wakaazi wakiongozwa na Daniel Lotuu alitoa wito kwa serikali kwa ushirikiano na kanisa kujenga shule katika maeneo hayo kwa lengo la kuwabadilisha mawazo ya vijana ambao anasema kuwa wanatumia visivyo kuzua vurugu na wale ambao wana nia yaoa ya kibinafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *