Wazazi wamehimizwa kuwaruhusu wanao kushiriki kikamilifu kwenye michezo mbalimbali shuleni kama njia moja ya kuwasaidia kuepukana na kujiunga na vikundi visivyostahili.
Akiongea afisini mwake mjini Eldoret,afisa mkurugenzi wa Elimu kaunti ya Uasin Gishu Khalif Hassan Isaac alisema kwamba maswala ya kimchezo shuleni huwapa fursa nzuri wanafunzi kuwa na mtazamo uliobora maisha na hawawezi kujihusisha na maswala yasiyowafaa.
Amesema kwamba kwa sasa mashindano mbalimbali shuleni zimerejeshwa hii ni baada ya kusistishwa kwa muda kufuatia mkurupuko wa virusi vya Corona.
Aidha,afisa huyo alitoa hakikisho kwamba shule chini ya mfumo mpya wa CBC za secondari msingi zimepokea pesa zilizokuwa zimetolewa na wizara kufanikisha shughuli zake.