Bikira Maria ni Mfariji

Ipo haja ya kila mkristu kumshirikisha Bikira Maria ambaye ni mwombezi  katika sala zao haswa wanapopitia changamoto za  maisha.

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo akihubiri katika misa ya daraja la upadirisho na lile la ushemasi wa shirika la mtakatifu Agustino, katika kanisa la mtakatifu Monika eneo la Njiro, askofu amewataka mapadre na mashemasi hao pamoja na wakristu siku zote kumshirikisha Bikira Maria akisema kuwa huyo Bikira ni daraja linalomuunganisha mkristu na kristu.

Amewataka wakristu siku zote kuombea miito mbalimbali akisema kuwa miito hiyo kadhalika huipa familia nyingi msingi wa sala, akitoa wito kwa kila mkristu kujisadaka bila kujibakisha katika safari kumtukuza mwenyezi Mungu.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *