Upendo nguzo muhimu katika familia

Wakristu wametakiwa kudhihirisha upendo wao kwa Mungu kwa kushiriki matendo yalioyomema siku zote haswa katika familia zao.

Akihubiri misa ya kusherehehea siku kuu ya moyo mtakatifu wa Yesu askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amewataka wanandoa kunogesha wito wao wa familia na kuuweka wito huo imara kwa kumncha Mungu na kuonyesha upendo huo ndani ya familian kupitia uaminifu.

Askofu Kimengich alisikitia swala la uaviaji wa mimba miongoni wale walio kwenye ndoa akiwakanya wale wanaoshiriki maovu hayo kukoma na kumrudia Mungu akikariri kuwa mtoto ni Baraka kutoka kwa Mungu.

Aliwatahadharisha vijana dhidi ya kukimbilia swala ya ndoa akisema kuwa wanastahili kuchukua muda na kumuusisha mwenyezi Mungu kabla ya kufanya maamuzi ya kuingia kwenye wito wa ndoa.

Kando na hayo askofu alitoa wito kwa familia kuombea miito mbalimbali akisema kuwa miito mbalimbali hukuzwa ndani ya familia, akielezea ufanisi wa miito jimboni ambayo kwa sasa imepelekea waseminaristi themanini na moja ikilinganishwa na majimbo mengine ambayo kwa sasa swala la wito wa kitawa unasalia kitendawili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *