Baba mtakatifu Francisko amelaani vikali shambulizi la kigaidi lililotekelezwa dhidi ya wanafunzi nchini Uganda siku ya Ijumaa.
Akizungumza alipoongoza misa ya Jumapili Baba mkatatifu amewakumbuka wanafunzi walioathirika kufuatia shambulio hilo ambalo limelaaniwa kote duniani.
Kwa mujibu wa polisi nchini Uganda ni kuwa takriban watu arobaini na wawili wengi wao wakiwa wanafunzi waliuawa siku ya Ijumaa katika shambulio baya zaidi kuwahi kutokea nchini Uganda tangu mwaka wa 2010.
Papa alizidi kuwatakia matashi mema wale waliopata jeraha kwenye shambulio hilo akitoa wito kwa wakristu wote walio na mapenzi mema kote duniani kuzifariji familia zilizopoteza wapendwa wao na kadhalika kuwaombea waliojeruhiwa.