Kuweni na imani dhabiti msitumbukie kwenye mauti

Wakristu wametakiwa kudhihirisha udhabiti wa imani yao katika kristu kwa njia ya matendo yanayonogeshwa kwenye amri za Mungu.

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret askofu Dominic Kimengich akihubiri katika parokia ya Nerkwo alisema kuwa sheria ya Mungu ndio mwongozo unaotoa mwanga kwa mkristu na kuimarisha imani yao, akitoa wito kwa wakristu kutoyumbishwa na wale wanaoneza imani potovu.

Aliwatahadharisha wakristu dhidi ya kuangukia mtego wa wale wanojitokeza na kujiita wahubiri, akisema kuwa nyingi ya mahubiri hayo hayana msingi, huku nia yao ikiwa tu ni ya kupotosha na lengo kadhalika likiwa ni la kujinufaisha wao wenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *