Kamati ya afya na ile ya fedha katika kaunti ya Nandi zimefanya vikao na washikdau mbalimbali ili katika sekta ya afya ili kujadili mikakati na umuhimu wa kuinua viwango vya lishe bora miongoni mwa watoto katika kaunti hiyo.
Wakizungumza mjini Kapsabet washikadau hao walisema kwamba viwango vya lishe bora viko chini sana kiasi cha kusababisha utapiamlo miongoni mwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Wadau hao walisema kwamba lengo kuu ni kushirikiana ni kuweka pesa za kutosha na kupambana na utapiamlo.