MKUU WA MABAWABU APIGWE KALAMU

Katibu wa chama cha wafanyikazi COTU tawi la kaunti ya Uasin Gishu Peter Odima amemtaka rais William Ruto kuingilia kati na kumpiga kalamu afisa mkurugenzi wa makampuni ya kibinafsi ya walinzi nchini Fazul Mohammed ambaye anasema wafanyikazi wanaendelea kunyanyaswa chini ya uongozi wake.

Akiongea mjini Eldoret,Odima alisema kwamba afisa huyo ameendelea kuwanyanyasa wafanyikazi katika muungano huo huku maswala tata yakikosa kuangaziwa kama ilivyokuwa kwenye makubalino.

Alisema kwamba Fazul amendelee kuzisajili makampuni ya walinzi wa kibanfsi kiholela bila kuzingatia kutimizwa kwa masharti na mahitaji ya wafanyikazi hao.

Odima alikariri kwamba mabawabu wengi chini ya uongozi wake afisa huyo wamendelea kuteseka kwa sababu wanapokea mishahara duni,kukosa bima ya afya na maswala mengine ya kimsingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *