Wito umetolewa kwa wakristu kuwaombea vijana kuitikia miito mbalimbali katika maisha yao.
Akiongea wakati wa hafla ya kusherekea miaka arobaini tangu kuanzishwa kwa parokia ya Mtakatifu Yosefu Mfanyikazi Njoro,askofu msimamizi wa jimbo katoliki la Nakuru askofu David Kamau kwamba ni vyema wanafamilia kukumbatia miito mbalimbali hasa wito wa kuhudumu katika shamba la bwana na kuendeleza neno lake mwenyezi mungu katika mataifa yote ulimwenguni.
Askofu vilevile,alisisitiza haja ya familia kukuza miito ya majandokasisi na wakleri na wasiwe wanaokatiza ndoto wana wao ambao wanalenga kujiunga na utumishi wa mungu.
Alisema kwamba iwapo jamii litaegemea tu kukuza miito mbalimbali na kupuuza wito wa utumishi wa mungu huenda changamoto zitakapojitokeza wanajamii watashindwa kusimama imara katika jamii na kuambilia katika mauti.
Kadhalika,askofu aliwaomba wakristu kuwa na hulka ya kutoa shukrani katika maisha yao kila mara kwa kila jambo ambalo wamejaliwa maishani huku akiwaeleza kwamba ni kupitia changamoto wanazopitia maishani imani ya kutoa shukrani inakuwa imara.