SHERIA YA MAKANISA ITEKELEZWE

Viongozi wa dini nchini wameikosoa serikali kwa kulegeza kamba katika usajili wa makanisa nchini.

Wakiongozwa na askofu mkuu wa jimbo katoliki kuu la Nyeri Anthony Muheria ni kwamba yapasa serikali kusimama kidete katika kutoa leseni kwa makanisa ndipo wale ambayo lengo lao kuu ni fiche litatupiliwa mbali huku akiwataka wakenya kupiga msasa makanisa na makundi ya kidini wanazojiunga nazo.

Muheria amesema haistahili kila mkenya anayekuja na wazo la kufungua kanisa anastahili kupewa nafasi au leseni kwa hili akisema itasaidia pakubwa katika kutupilia mbali madhehebu ambayo inaenda kinyume na mafundisho ya kristu.

Kauli ambayo imeungwa mkono na naibu msimamizi wa kanisa All Saints Cathedral Evans Omollo ambaye amesema kwamba haistahili kutumiwa vibaya uhuru wa kujieleza akisema kwamba katiba ipo kuwaelekeza wakenya kwenye njia salama na sio za kupotoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *