Wito umetolewa kwa wazazi kukuza talanta za wanao ndipo waweze kuwa na msingi bora katika maisha ya hapo baadae.
Kwa mujibu wa Moses Kebenei ambaye ni mwakilishi wadi ya Simat/Kapseret kaunti ya Uasin Gishu ni kwamba talanta nyingi zimefichwa kwa sababu baadhi ya wazazi kukosa kuwashika wanao mikono katika kuwainua watoto wao katika kuafikia malengo yao ya maisha hasa ya kimechezo.
Mwakilishi huyo alisema kwamba yapo baadhi ya sera ambazo wadi hiyo imeweka angalu vijana wapate mahala pa kunoa makali ya michezo waliobobea nazo akiwahimiza kutumia vyema nafasi hizo katika kuwaimarishia wanao maisha bora hata zaidi.
Alisema kwamba yastahili wenyeji kutumia maeneo yaliyotengwa kama vile viwanja mbalimbali katika kukuza michezo iwe riadha au hata aina mbalimbali ya michezo ambazo wanao wanazienzi.