Wazee kutoka jamii ya kalenjin katika kaunti ya Uasin Gishu wameitaka serikali ya kitaifa kupitia wizara ya usalama wa Ndani kuwahusisha wazee katika maswala ya kutafuta suluhu la kudumu kuhusiana na utovu wa uslama unaoshuhudiwa katika Bonde la Kerio.
Wakiongozwa na Major John Seii wazee hao walisema wazee wanayo nafasi kuu katika uongozi katika jamii na iwapo wizara itawaruhusu kuwa mojawapo ya watu wanaosaidia kupatikana kwa suluhu wanafaa kujumuishwa akisema oparesheni ya kutwaa silaha haramu itafua dafu iwapo wazee kutoka jamii hizo watafikiwa.
Seii alisikitikia hali ambayo wenyeji maeneo yanayopatakana na Kerio wakipoteza maisha,wengine wakisali bila makao na hata ikiwasababishia wao kuishi kwa uwoga ,amebaini kwamba wazee huenda wakawa na suluhu la kudumu.