Wizara ya barabara ,uchukuzi na ujenzi wa umma katika kaunti ya Uasin Gishu imetenga magari ya ujenzi mawili kwa kila kaunti ndogo ili kufanikisha kwa haraka shughuli za ukarabati wa barabara katika kaunti nzima.
Kulingana na waziri wa idara hiyo Mhandisi Joseph Lagat ni kwamba zaidi ya kilomita 800 ya barabara hadi sasa zimeboreshwa katika muda wa miezi mitatu tangu kuzinduliwa kwa mradi wa ujenzi na ukarabati huo.
Lagat vilevile alisema kwamba wanapanga kukamilisha kuweka changarawe kwa barabara hizo kabla msimu wa mvua nyingi kuwadia ili kurahisisha usafiri mashinani.
Kadhalika,aliweka wazi kwamba wizara inalenga kuwapa mafunzo kwa mafundi na watendaji wote ili kuwapa ujuzi zaidi wa maswala ibuka katika Nyanja za teknolojia ya kisasa na mashine mpya sokoni.