Muungano wa wahudumu wa Afya katika kaunti ya Elgeyo Marakwet wametishia kusitisha huduma za afya katika eneo la Kerio Valley iwapo serikali haitaingilia kati kwa haraka na kutoa suluhisho kamili kuhusiana na uvamizi wa mara kwa mara.
Kulingana na katibu wa maafisa wa kliniki katika kaunti hiyo Mark Kipsang ,kisa hicho ni Cha kuhuzunisha akitaka serkali kuingilia kati kwa haraka swala hilo jambo ambapo aliungwa mkono na katibu wa wauuguzi Benson Biwot.
Haya yanajiri siku moja tu baada ya wahudumu wawili wa afya kuuwawa kwa kupigwa risasi na wavamizi ambao wanaaminika kuhusika na wizi wa mifugo katika eneo la Arror na Endo.