Mwanzilishi wa mbio za Eldoret City Marathon Moses Tanui ameweka wazi kwamba washindi wa awamu ya tatu ya mashindano hayo mapema mwaka jana watalipwa ijumaa hii.
Akiongea na wanahabari Mjini Eldoret,Tanui alisema lengo lao kuu kuanzishwa Kwa mashindano hayo ni Kwa vijana kuimarisha talanta zao na hivyo nia ya kuwasaidia kujikimu kimaisha kupitia mbio hizo.
Amewaomba radhi walioshiriki mashindano hayo kwa kugawia Kwa malipo hayo akiashiria hali mbaya ya uchumi wa nchi ilichangia pakubwa kucheleweshwa Kwa malipo hayo.
Aidha,Tanui aliwashukuru wanariadha Kwa kujituma kimaisha na kuinua taifa hili kupitia riadha na kuuza jina la Kanya.
Kadhalika Tanui ambaye alikuwa mwanariadha tajika nchini aliweka bayana kwamba lengo lake kuu kuanzishwa kwa mashindano hayo ni kuwainuwa wanariadha wanaochipuka akiwataka wao kujituma na kujitenga na maswala yasiyokuwa na mwelekeo.
Ikumbukwe kuwa mbio za Eldoret City ziliandaliwa mwaka jana Aprili na washindi hawakua wamelipwa pesa zao huku wa kwanza alikuwa ameingiza mfukoni shillingi million tatu nukta tano.