Viongozi wa dini ya kiislamu ukanda wa kaskazini mwa bonde la ufa wamemtaka rais William Ruto kuvunja kimya chake na kutoa msimamo wake kufuatia maamuzi yaliyotolewa na mahakama ya upeo yaliyoipa mashoga uhuru wa kutangamana.
Mwenyekiti wa baraza la maimam kaskazini mwa bonde la ufa CIPK sheik Abubakar Bini amesema kuwa dini ya kiislamu kamwe haitaridhia uamuzi huo na kwamba wataendelea kuipinga, wakisema kuwa uamuzi huo unanuia kupotosha jamii, ikizingatiwa kwamba kukubaliwa kwa ndoa ya jinsia moja ni kinyuma na maadili ya jamii.
Kiongozi huyo kadhalika ametoa wito kwa rais William Ruto kutonyamaza na badala yake kuiga mfano wa jirani yake wa nchi ya Uganda Yoweri Museveni ambaye ametia sahihi sheria ya kuharamisha hulka hiyo.
Haya yanajiri siku chache tu baada ya baraza hilo na maimam kutishia kuandaa maadamano tarehe kumi na saba mwezi wa tatu iwapo uamuzi huo hautabatilishwa