hatutakiuka maadili yetu

Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim amekosoa vikali hatua ambayo mahakama ya Rufaa kuidhinisha kibali ya wasagaji kuwa huru kuidhinishwa kama vyama vingine vya kijamii  humu nchini.

Gavana Chelilim alisema haya ni kinyume na mafundisho matakatifu ya bibilia ambapo maswala ya jinsia moja kukubaliwa akiitaka korti kuichunguza upya uamuzi wake ndio wenyeji waweze kuendelea na mwongozo uliobora wa maisha na wa kiafrika.

Chelilim ameeleza kwamba kibali hicho kitachangia pakubwa vijana wengi kupotoka kimaadili na huenda wengi wao wakasahau maadili ya kijamii na kuharibika kwa kizazi kijacho ambacho amesema hakitakua na mwelekeo uliodhabiti.

Aliwataka viongozi wa kanisa kusimama kidete kurejesha hadhi ya kanisa kwa njia inayompendeza mungu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *