MUREITHI:Dumisheni ushirikiano wenu na maafisa

Wito umetolewa kwa wenyeji katika kaunti ya Uasin Gishu kuhakikisha kwamba wameshirikiana kikamilifu na idara ya usalama ndipo amani iweze kudumu katika maeneo yao na Kaunti nzima kwa jumla.

Kulingana na kamanda wa polisi katika kaunti ya Uasin Gishu Moses Mureith ni kuwa ni kupitia ushirikiano  tu ndipo wakaazi waweze kuishi kwa amani maana watakuwa tayari kuwatambua wahalifu na kuziba mihanya yote ambayo magenge ya wahalifu ingetumia kuwanyima usingizi wenyeji.

Kamanda huyo alisisitiza haja ya wananchi kuwa tayari kuwa karibu na maafisa wa usalama akiwathibitishia kwamba wao ni binadamu tu ila walipata jukumu kuwahudumia wenyeji waweze kulinda mali yao kwa njia mwafaka kwa kuwakabili wahalifu.

Alisema kuwa wamepanga na viongozi wa nyumba kumi na wazee wa mitaa pamoja na idara nzima ya usalama kuwahakikishia wenyeji usalama kila mara na waweze kuishi bila ya uwoga wowote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *