Vijana muepuke madawa za kulevya

Askofu wa jimbo katoliki la Kitale Henry Juma Odonya ametoa wito kwa vijana kujiepusha na mihadarati na badala yake kumrejelea mwenyezi Mungu na kufanya kazi yake katika miito mbalimbali.

Akiongea na idhaa hii askofu Juma alisema kuwa visa vya matumizi ya mihadarati miongoni mwa vijana vimechangiwa na ukosefu wa uwajibikaji wa wazazi pamoja na walezi walio na jukumu la kuwalea vijana hao, akitoa wito kwa jamii kujitokeza na kuchukua jukumu hilo la malezi ili kuokoa kizazi kijacho.

Askofu Odonya alihaidi kushrikiana na vijana katika jimbo la Kitale na kuwashirikisha katika maswala tofauti kama njia moja ya kuzuia kusambaa kwa hulka hiyo miongoni mwa vijana.

Ametoa wito kwa jamii kwa ujumla kushirikiana na idara mbalimbali ikiwemo shule kanisa na hata idara mbalimbali ili kuokoa kizazi kijacho dhidi ya mihadarati.

Askofu kadhalika aliangazia swala la amani katika eneo la Kerio akitoa wito kwa wale wanaoishi katika maeneo hayo haswa wakaazi wa kaunti ya Pokot Mgharibi iliyoko chini ya jimbo katoliki la Kitale kukumbatia amani kama njia moja ya kufanikisha miradi ya maendeleo maeneo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *