Kueni watiivu katika shamba la bwana

Wito umetolewa kwa makleri kuwa wenye unyenyekevu wanapotekeleza jukumu lao ndipo waweze kuwaongoza wengine vyema katika kutwaa uzima wa milele.

Akiongea wakati wa misa ya daraja la  upadrisho katika jimbo katoliki la Bungoma,askofu wa jimbo la Bungoma Mark Kadima amesisitiza haja ya viongozi hao kuwa mfano mwema kwa wengine na kuwa wenye matendo ya kuigwa.

Aidha,askofu Kadima aliwataka mapadre hao kuwa tayari kufanya kazi na viongozi wengine kanisani pamoja na wakristu akisisitiza kwamba hakuna mafanikio yatakayopatikana ijapokuwa kupitia washiriki kanisani kuungana mikono na kutekeleza majukumu yao ya ukristu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *