Kaunti ya Uasin Gishu imetayarisha maghala matano ya kuhifadhi na kusambaza mbolea kwa wakulima wote katika kaunti nzima.
Kulingana na waziri wa kilimo katika kaunti hii ya Uasin gishu Edward Sawe amesema kuwa hii itakuwa njia bora ya kuzuia wakiritimba walio na lengo la kuwanyanyasa wakulima kwa kuwauzia mbolea hiyo kwa bei ghali.
Sawe kadhalika alisema kuwa mghala hayo matano yana uwezo wa kuhifadhi mbolea gunia elfu sita na itauzwa kwa shilingi elfu tatu mia tano kwa kila gunia.
Waziri huyo alisema kuwa kufikia sasa wakulima wapatao elfu mia tisa kwenye kaunti hii tyari wamejisajili katika sajili za kaunti kulingana na utaratibu uliowekwa
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya bodi ya kuhifadhi mazao na nafaka kwenye ukanda wa NORTHRIFT gilbert Rotich amewahakikishia wakulima kuwa kutakuwa na mbolea ya kutosha haswa katika kipindi cha upanzi.