Madhehebu kushirikiana katika kufanikisha amani

Wito umetolewa kwa wakristu wa madhehebu mbalimbali kushirikiana na kutembea pamoja kama njia moja ya kutatua changamoto ambazo zinakumba jamii kwa ujumla.

Askofu wa jimbo la Kitale Henry Juma aliwataka wakristu siku zote kushirikiana kwa pamoja bila kuweka mipaka ya dini ili kutatua changamoto nyingi ambazo zinakumba jamii kama vile ukosefu wa amani, matumizi ya mihadarati miongoni mwa vijana na hata maswala yanayohusu maendeleo ya jamii.

Askofu Juma alikiri kuwa kumekuwapo na ubaguzi kwa misingi ya dini jambo analosema linastahili kuangaziwa kwa kina, akisema kuwa changamoto zinazowakumba wasio na imani ya kikristu ni sawia na zile ambazo zinawakumba walio na imani ya kikristu, akitoa wito kwa kila moja kushiriki meza ya mashauriano kuhusu mambo ambayo yatanufaisha jamii.

Alisema kuwa hakuna changamoto zisizokuwa na suluhu ila binadamu wametengana kwa msingi huo wa kidini, akisema kuwa ipo haja ya wakenya wote walio katika madhehebu mbalimbali kushirikiana na kutatua changamoto ambazo kwa sasa zinalemaza shughuli nyingi za maendeleo nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *