serikali ya Uasin Gishu kukarabati barabara Eldoret

Wakulima kwenye kaunti ya Uasin gishu  hivi karibuni watasafirisha mazao yao sokoni  kwa wakati baada ya serikali ya kaunti kuzindua mpango wa kukarabati barabara katika wadi zote kwenye kaunti hiyo.

Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim akiongea kwenye hafla ya kuzindua  barabara ya Merewet  iliyoko kwenye wadi ya Soy, amekariri kuwa serikali yake ina mpango wa kuhakikisha kuwa barabara kwenye wadi zote zimewekwa lami na halkadhalika kusafisha mitaro yote iliyozibwa na taka kama njia moja ya kuzia mafuriko kwenye barabara wakati wa mvua.

Baadhi ya barabara zitakazokarabatiwa kwa ushirikiano na mamlaka ya kukarabati barabara za miji nchini  KURA ni pamoja na barabara ya Bandaptai na ile ya Famers, serikali ikihaidi kuweka mahali pa kutembelea kwa wale watakaotumia miguu ni ile Saroiyot  miongoni mwa barabara zingine mjini Eldoret.

Mkurugenzi mkuu wa KURA Silas Kinoti amesema kuwa hatua kukarabati barabara hizo kadhalika zitasaidia  kupunguza msongamano wa magari , nah ii itasaidia na kufanikisha bidhaa nyingi kufikishwa sikoni kwa wakati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *