Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ametoa wito kwa wakaazi wa bonde la Kerio kukumbatia amani, akisema kuwa hali ya utulivu katika eneo hilo ndiyo itawapa mazingira ya kufanya miradi mbalimbli ya maendeleo.
Katika kikao na wanahabari mjini Iten askofu Dominic Kimengich ametoa wito kwa kila mkaazi wa eneo hilo kuhubiri amani na kukoma kulipisha kisasi, akisema kuwa hulka hiyo imelemaza shughuli mingi maendeleo na wengi wakibaki mayatima na wajane kufuatia vita hivyo.
Askofu kadhalika ametoa wito kwa wale wanaomiliki silaha haramu katika eneo hilo, kusalimisha silaha hizo kwa idara husika, akitoa wito kwa jamii zote katika eneo hilo kushiriki mdahalo ya kufanikisha maridhiano miongoni mwa pande husika.
