UFADHILI WA KUJIINUA KIMAISHA

Wenyeji katika kaunti ya Uasin Gishu wamehimizwa  kujitokeza kubaini baadhi ya makundi yenye hitaji ya kimsingi hasa Shule,hospitali au vikundi vya kimaendeleo ndipo viweze kufaidika na mradi wa kuwainua kimaisha kwenye vikundi.


Kulingana na meneja wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom tawi la Uasin Gishu Sara Choge ni kwamba,kupitia wakfu ya Ndoto zetu ambayo kampuni hiyo imebuni,inaendelea na juhudi zake za kuwainua watu wa kiwango cha chini katika jamii na kuwawezesha kimaisha na pia kusambaza madawati ,viti katika zahanati kadhaa zilizotambuliwa.

Aidha,meneja huyo amesema kwamba wanapania kuendelea na shughuli hiyo baada ya kukamilika Kwa awamu hii ya kwanza ambapo watafungua nafasi Kwa wenyeji kujisajili kama wale watakaofaidika na ufadhili wa aina yoyote Ile.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *