Serikali ya kaunti ya Elgeyo Marakwet imepokea mashine kutoka shirika la huduma ya kitaifa kwa vijana ambalo litasaidia kufungua barabara katika maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo.
Akiongea baada ya kupokea mashine hizo gavana wa kaunti hiyo Wesley Rotich amesema kuwa bado wanatarajia mashine zingine zitakazotumika kukarabati barabara katika maeneo bunge zote manne za kaunti hiyo .
Rotich aidha alidokeza kuwa hatua hiyo itawasaidia wakazi hasa kusafirisha bidhaa zao sokoni na kuboresha shuguli za uchukuzi hasa kwa maafisa wa usalama wanaoendeleza oparesheni katika maeneo ya bonde la Kerio.