Visa vingi vya mtoto kukosa kuongea akiwa mtu mzima huchangiwa na wazazi kutelekeza jukumu lao la kuwapa mazoezi wanao wanapokuwa wachanga.
Haya ni kwa mujibu wa Mtawa Gladys Chepkemei wa shirika la Assumption Sisters ambaye ni mmoja wa watu wachache walio na uwezo wa kuzungumza na watoto wasikuwa na uwezo wa kuongea na alieleza kwamba iwapo wazazi watachukua jukumu la kuwa karibu na wanao kila muda watasaidia katika kuimarisha ukuaji mzuri wa wanao kimaongezi.
Mtawa Gladys alidokeza kwamba wazazi wanastahili kuwa mstari wa mbele kutambua kile wanachopitia wanao isije wakajipata katika njia panda ya kuwalea watoto wasioweza kuongea akieleza kwamba mtoto asipokua na uwezo wa kujieleza hujulikana mapema na wawaeze kusaidika mapema na wengine wanajipata kushindwa kuongea kwa kukosa mawasiliano mazuri na wanaomlea.
Amesema kuwa hamasisho la kutosha yastahili kwa jamii kuwakumbatia watoto hao na kuwasaidia kujieleza kwao akisema watoto hao ni Baraka mradi tu jamii kuwaelewa na kuwapa mapenzi.
Mtawa huyo kadhalika alibainisha kwamba ni jukumu la kila mmoja katika jamii kuwa mstari wa mbele kuwabaini watoto wasikokua na uwezo huo na kuwasaidia wakiwa wadogo ndipo maisha yao ya baadae iwezi kujengwa.