Serikali ya Kaunti ya Uasin Gishu imesema imeimarisha vita dhidi ya pombe haramu katika oparesheni ambayo inaendeshwa na maafisa wa ukaguzi katika wadi ya Kuinet Kapsuswa kaunti ndogo ya Soy.
Akiongea wakati wa kusimamia shughuli hiyo katika eneo la Kuinet,kaimu mkurugenzi wa bodi ya kudhibiti vinywaji kaunti ya Uasin Gishu Koiya Maiyo aliwataka wakaazi hao kuwa mstari wa mbele katika kubainisha maeneo ya kutengeneza pombe kwa vile imeathiri maisha yao na kizazi kijacho.
Alisema kwamba jumla ya lita 600 za pombe aina ya kangara na lita 50 za changaa zilinaswa.
Oparesheni sawia ilifanyika katika eneo la Sugunanga katika wadi ya Racecourse kaunti ndogo ya Kesses ambapo wafanyibiashara zaidi ya 15 walinaswa na pombe haramu na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Afisa huyo akisema wataendeleza oparesheni hiyo hadi pombe haramu imalizwe.