Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo amezitaka familia kudumisha upendo wao kwa baraka ya watoto walio jaliwa na kutotelekeza jukumu lao la uzazi.
Akiongea katika kanisa la Parokia ya Mtakatifu Yosefu Loreto Limuru Askofu Anyolo alisema jukumu la malezi sio tu kwa mama au baba pekee bali ni kwa wazazi wote wawili kando na jamii kuwapa mwelekeo watoto hao kwa maisha yanayowaelekeza katika mwanga.
Amewataka kuboresha imani yao kwa wanao ndipo waweze kuwa na uepesi wa kuelewa changamoto wanazopitia na kuwaepusha na vikundi visivyofaa kwa wanao ambazo amesema huenda ikaatarisha hulka za wanao na kupotoka kimaadili.
Wakati huo Askofu Anyolo alisisitiza haja ya kuwapokea baraka ya watoto waliotunukiwa na mungu kwa maana hakuna kiumbe kilichoumbwa na mungu ambacho hakina umuhimu.