matokeo bora ya kcpe imetokana na kujinyima kwa watahiniwa

Shule mbalimbali za msingi katika kaunti ya Uasin Gish Zimepokea matokeo bora kutoka kwa watahiniwa wake ambao walikua kati ya watahiniwa million 1.2 waliofanya mtihani wao wa kitaifa KCPE.

Katika shule ya msingi ya Gatesmani na shule ya msingi ya Hill school viungani mwa mji wa Eldoret mwanafunzi bora alizoa alama 420 ikiwa na wanafunzi zaidi ya 15 waliozoa alama 400 kuendelea .

Wanafunzi hao walieleza kwamba kujituma kwao na ushirikiano mwema kati yao,walimu ,wazazi na hata jamii imefanikisha matokeo hayo bora.

Wamewarai wenzao kutokata tamaa katika maisha kwani kila mmoja wao analo nyota lake la maisha.

Hesbon Ngaira ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya hillschool alibainisha kwamba nidhamu na kujituma kwa wanafunzi ilifanikisha matokeo bora ambapo watahiniwa zaidi ya 15 walikizoa alama ya mia nne na zaidi.

kulingana na data za wizara ya Elimu nchini,kati ya watahiniwa millioni 1.2 waliofanya mtihani wa kitaifa kcpe wavulana walikuwa 620,965 hii ikiwa asilimia 50.32 huku 612,887 ya asilimia 49.67 ikiwa ya wasichana .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *