Sherehe za krismasi na mwaka mpya zikiwa zimeshika kasi katika maeneo tofauti humu nchini baadhi ya wakazi wa kaunti ya Uasin Gishu sasa wanasema hawasafiri kuelekea sehemu za mashambani ili kujumuika na familia zao kusheherekea sikukuu hiyo kufuatia hali ngumu ya kiuchumi.
Wakazi hao ambao wanatoka katika kaunti zingine wanasema kwamba gharama ya juu ya usafiri imewazuia kwenda mashambani na hivyo wamemua kuendelea na kazi zao ili waweze kujipanga kutafuta karo ya shule ya mwaka ujao.
Wakizungumza mjini Eldoret wanaitaka serikali kuweka mikakati ya kuteremsha bei ya mafuta wakisema kwamba imechangia pakubwa kupanda kwa gharama ya maisha.