Naibu Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu John Barorot amesema kwamba serikali ya kaunti imeweka mikakati za kutosha kuhakikisha usalama umeimarishwa msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya.
Akiongea mjini Eldoret ,Barorot alisema serikali ya Kaunti ikishirikiana na idara ya usalama imewaka sera za kudumu kwa kuwepo maafisa wa usalama wa kutosha na kueleza kwamba hakuna sababu za wenyeji kuhofia usalama wao.
Wakati huo aliwashauri madereva kuwa waangalifu na kutoongeza nauli kwa wateja wao kwa kile amesema wateja hao ndio watakao wahitaji baada ya msimu wa sherehe.