ASKOFU KIMENGICH:Jamii ichukue fursa yake kuwaelekeza watoto

Askofu wa dyosisi ya Eldoret Dominic Kimengich aliwataka wazazi na jamii kwa ujumla kuwa karibu na watoto ndipo maswala ya utovu wa kinidhamu na maswala mengine yanayoathiri hulka za watoto kukabiliwa.

Akizungumza afisini mwake mjini Eldoret,askofu Kimengich alisisitiza haja ya kuwa na uamkini kwa vijana hao wasije wakajiingiza kwenye mambo ya usherati kutokana na marafiki ambao wanawapotosha msimu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya ukiwa umewadia.

Vilevile,askofu Kimengich akiwashauri madereva dhidi ya kuvunja sheria za  barabarani na unywaji wa pombe kuwa haistahili na wanafaa kujukumika ndipo maisha ya wasafiri na wateja wao iwe salama na wafike wanako elekea wakiwa salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *