Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo ametoa wito kwa waumini kujiunga na kwaya mbalimbali katika parokia zao akisema kuwa uimbaji ni njia moja ya kujenga liturjia ya kanisa.
Askofu mkuu Anyolo amesema kuwa kuwa kwaya ni chombo maalum katika uenezwaji wa injili na ni njia mwafaka wa kukuza injili ndani na nje ya nchi.
Ametoa wito kwa wanakwaya kadhalika kuendelea kueneza injili haswa wakati huu kwaya inaposherehekea siku ya mtakatifu Cecilia ambaye ni msimamizi wa kwaya zote.