DG BAROROT:Kufungwa kwa soko

Ni wazi sasa kwamba soko kuu ya chakula katikati mwa mji wa Eldoret itasilia mahame kwa siku saba zijazo kufuatia rabsha zilizoshuhudiwa mapema jana wakati baadhi ya maduka yakiporwa kutokana na kizaazaa kilichoshuhudiwa huku serikali ya kaunti ikisema inaweka mikakati za kuimarisha amani sokoni.

Kulingana na naibu gavana wa kaunti ya Uasin Gishu mhandisi John Barorort ni kwamba hatua hiyo imetokea baada ya maafisa kutoka idara ya usalama na wakuu wa kaunti kuandaa mkutano na kujadiliana mbinu za kurejesha amani na wafanyibiashara kuendelea na biashara zao.

Wafanyibiashara aliwahimizwa kutumia soko nyiningeyo katika kaunti ya uasin gishu kuendeleza biashara zao kwa wakati huo wa kuwekwa kwa mikakati za yupi anastahili kuwepo sokoni kulingana na sheria za kaunti.

Kadhalika,barorot alieleza kwamba wachuuzi wanaotumia mkokoteni wa kisasa maarufuku bangbang hawatakuwa na nafasi sokoni kwa kile anasema uhaba wa nafasi kwa shughuli zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *